Tasfida kama sababu ya Siti binti Saad kutumia mafumbo katika nyimbo zake za taarab

  • Juma, Job
Publication date
April 2022
Publisher
Royallite Global

Abstract

Makala hii inaangaza sababu iliyomsukuma Siti kuishia kutumia mafumbo katika nyimbo zake za Taarab. Sababu yenyewe ni mafumbo kama njia mojawapo ya kuendeleza lugha ya tasfida na miiko katika jamii au mafumbo kama njia moja ya mwimbaji kupamba lugha yake ya uimbaji. Lugha hupambwa kwa mafumbo ili wasikilizaji waweze kuifurahia na kuikumbatia. Siti aliremba nyimbo zake kwa ufundi wa tasfida. Mihimili ya nadharia ya Semiotiki na Mtindo ilitumika katika uchanganuzi wa data. Data za msingi zilipatikana kwa kutumia mbinu ya mahojiano na kwa kusikiliza nyimbo. Wafuasi wa nyimbo hizi kutoka Mombasa na Unguja walihojiwa ili kupata ujumbe mahususi kuhusu nyimbo hizi za Siti Binti Saad. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Makala ha...

Extracted data

We use cookies to provide a better user experience.